Imaam Ibn Abiy Haatim ar-Raaziy (afk. 327) amesema:
“´Aqiydah yetu na chaguo letu ni kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake na wale waliokuja baada yao waliowafuata, kushikamana barabara na madhehebu ya Ahl-ul-Athar, akiwemo Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal, Ishaaq bin Raahuuyah, Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam na ash-Shaafi´iy, na kushikamana na Qur-aan na Sunnah. Tunaamini kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake na ametengana na viumbe Wake.” (Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 184)
Dhumuni la tovuti ni kutumika kama balozi wa wanazuoni. Makala za tovuti zinafanyiwa tarjama kutoka katika vitabu vya kiarabu, sauti na mahojiano ya mdomo na wanazuoni. Kunaweza kuwekwa baadhi ya ziada kama vile maelezo ya chini n.k., lakini ni kitu ambacho hubainishwa.