Swali: Kuko ambao wako katika Chuo Kikuu wanachukua elimu, lakini anataka kujua hukumu ya Uislamu, naye amechanganyika na wanawake, kwa kuwa masomo katika Chuo Kikuu hichi ni ya mchanganyiko, yaani ni wanaume na wanawake. Na wanawake wengi katika Chuo Kikuu hichi sio wenye kujisitiri na wanavaa nguo zinazoonesha.

Jibu: Nasaha zetu kwa huu mwanafunzi ni kwamba asisome na wanafunzi wakike na wala asichanganyike nao. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika kufitinika nao. Ni juu yake atafute njia nyingine ya kujifunza. Ama kusoma na wasichana, hakika hii ni njia inayopelekea katika khatari kubwa. Ni wajibu kwake kutahadhari na hilo. Masomo ya mchanganyiko yana shari kubwa na ufisadi mkubwa. Na wala haijuzu kwa mtawala kulichukulia sahali. Bali ni wajibu kwa watawala masomo yasiwe mchanganyiko. Namna hii ndio inapaswa kuwa, watawala wa Waislamu ni wajibu kwao kufanya masomo ya wanawake yawe upande wake pamoja na ulinzi na kuhifadhiwa, na masomo ya wanavulana yawe upande wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 01/02/2024