Swali: Mwandishi wa “Manhaj-ul-Anbiyaa´ fiyd-Da´wah ilaa Allaah” amesema:

“Nimesoma vitabu vya ´Aqiydah na kuona kuwa vyote si vyenye kuridhisha. Kwa sababu vina Hadiyth tu, maandiko na hukumu.”

Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hili ni kosa kubwa. Vyote haviridhishi? Namuomba kinga Allaah. Vitabu vya ´Aqiydah sahihi sio vyenye kuchosha. Humo mnanukuliwa aliyosema Allaah na Mtume Wake. Ikiwa anamaanisha kuwa Qur-aan na Sunnah ni vyenye kuchosha huku ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Maneno haya ni ya kigonjwa na machafu.”

Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza kitabu hiki?

Jibu: Ikiwa mna maneno haya haijuzu kukiuza. Ni wajibu kukipasua ikiwa maneno hayo yamo humo.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara “Aafaat-ul-Lisaan”, 1413-12-29, uliofanywa Twaaif