28. Mume kuhakikisha anamfikisha mke kileleni na anamjamii ipasavyo

Isitoshe mume anatakiwa asimuharakishe mke wake pindi yeye anapomaliza matamanio yake. Asiwe mbinafsi ambaye hakuna anachojali isipokuwa tu yeye kutekeleza matamanio yake. Kwani hakika mwanamke anayahisi yale anayohisi mwanaume katika furaha, raha na matamanio. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatuongoza katika hayo na haya haikumzuia kubainisha. Kwa hivyo sisi tunaigiliza Sunnah zake.

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mmoja wenu anapomjamii mke wake basi amfanye kikweli. Halafu anapomaliza haja yake kabla ya yeye kumaliza haja yake, basi asimuharakishe mpaka naye amalize haja yake.”[1]

al-Munaawiy amesema alipokuwa akiitolea maelezo Hadiyth hiyo:

”Anapomjamii mmoja wenu mke wake basi amjamii kwa nguvu, afanye uzuri kile kitendo cha ndoa, mapenzi na kumtakia mema. Akimtangulia mke wake katika kumwaga na ilihali yeye mwanamke angali na matamanio, basi asimuharakishe. Kwa maana ya kwamba asimfanye kufanya haraka ikawa hatomaliza matamanio yake. Bali ampe muda mpaka naye amalize haja zake kama ambavo yeye amemaliza haja zake. Asikae naye mbali mpaka imbainikie kuwa naye amemaliza haja zake. Hakika kufanya hivo ni katika uzuri wa kuchanganyika, kujichunga na machafu, kujipamba na kumfanyia tabia njema na upole.”

Kumepokelewa nyongeza, kama ilivyo katika ”al-Washshaah”:

”Pamoja na sitara, kumnyonya mdomo na kupapasa matiti.”[2]

al-Albaaniy amesema katika ”al-Irwaa´”:

”Hadiyth ya Anas ni kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Humo imekuja pia:

”Kisha akimaliza haja zake, basi asimuharakishe mpaka naye amalize haja zake.”

Ameipokea Ahmad, Abu Hafsw na akaashiria juu ya unyonge wake.”[3]

al-Munaawiy amesema:

”Tunachofaidika katika Hadiyth hii na yanayofuatia baada yake kwamba mwanaume akiwa ni mwenye kumaliza haja yake haraka kwa njia ya kwamba hawezi kumpa muda mke wake mpaka na yeye amalize haja zake, inasuniwa kwake kujitibisha kwa mambo yatayomcheleweshea yeye kumaliza haja yake. Kwa sababu hiyo ni njia inayopelekea katika kilichosuniwa – njia zina hukumu moja na yale makusudio.”[4]

Ibn Qudaamah amesema katika ”al-Kaafiy:

”Akimaliza kabla yake, basi inachukiza kwake kuchomoa mpaka naye amalize kutokana na yale aliyosimulia Anas… ”

na akataja ile Hadiyth yake iliyotangulia.”[5]

[1] Abu Ya´laa katika ”al-Musnad” yake (07/208). Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (451).

[2] Faydhw-ul-Qadiyr (01/418) ya al-Munaawiy.

[3] Irwaa´-ul-Ghaliyl (01/71).

[4] Faydhw-ul-Qadiyr (01/418) ya al-Munaawiy.

[5] Tazama ”al-Kaafiy fiy Fiqhi Ibn Hanbal” (03/81) ya Ibn Qudaamah al-Maqdisiy.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 44-46
  • Imechapishwa: 25/04/2024