04. Kuweka mkono juu ya bibi harusi na kumuombea du´aa

2- Kuweka mkono juu ya kichwa cha mke na kumuombea du´aa

Mwanaume anatakiwa kuweka mkono wake juu ya kichwa chake wakati wa kufunga ndoa au kabla ya kumwingilia na kumtaja Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na kuomba baraka na aseme yale yaliyopokelewa katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakapooa mmoja wenu mwanamke au akamnunua kijakazi, basi aweke mkono wake sehemu ya mbele ya kichwa kisha amtaje Allaah (´Azza wa Jall) na aombe baraka hali ya kusema:

اللهم إني أسألك من خيرها وخير ما جبلتها عليه وأعوذ بك من شرها وشر ما جبلتها عليه

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba katika wema wake na wema wa Uliyomuumbia na najilinda Kwako kutokamana na shari yake na shari Uliyomuumbia.”[1]

na akinunua mnyama [kipando], atamshika kichwa chake na kisha atasema mfano wa hivo[2].

[1] Katika Hadiyth hii kuna dalili inayofahamisha kwamba Allaah ndiye muumbaji wa kheri na shari tofauti na wale Mu´tazilah na wengineo ambao wanaonelea kuwa shari haikuumbwa na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Kule kusema kuwa Allaah ndiye kaumba shari hakupingani na hekima Yake (Ta´ala). Bali ni katika ukamilifu Wake. Ufafanuzi wa hilo ni vile vitabu vikubwa. Miongon mwa vitabu bora ni kitabu “Shifaa´-ul-Ghaliyl fiyl-Qadhwaa´ wal-Qadar wat-Ta´liyl” cha Ibn-ul-Qayyim. Arejee huko yule anayetaka. Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah mtu kusoma du´aa hii wakati wa kununua kwa mfano gari? Ndio, kutokana na ile kheri inayotarajiwa kwayo na shari inayochelewa kwayo.

[2] Ameipokea al-Bukhaariy katika “Af´aal al-´Ibaad”, uk. 77, Abu Daawuud (01/336), Ibn Maajah (01/592), al-Haakim (02/185), al-Bayhaqiy (07/148), Abu Ya´laa katika “al-Musnad” yake (02/308) kwa mlolongo wa wapokezi mzuri. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana naye. al-Haafidhw al-´Iraaqiy amesema:

“Mlolongo wa wapokezi wake ni mzuri.” (Takhriyj-ul-Ihyaa´ (01/298)).

´Abdul-Haqq al-Ishbiyliy ameashiria juu ya usahihi wake katika “al-Ahkaam al-Kubraa” (02/42). Vivyo hivyo kafanya Ibn Daqiyq al-´Iyd katika “al-Imaam” (02/127).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 23/02/2018