Swali: Je, inajuzu kwa wanaume kuimba Anaashiyd za Kiislamu? Je, inajuzu kuwapigia dufu wanapoimba? Je, inajuzu kuimba Anaashiyd mbali na sikukuu na sherehe?

Jibu: Anaashiyd za Kiislamu ni Anaashiyd zilizozushwa. Zimeshabihiana na waliyozusha Suufiyyah. Kwa hivyo inatakiwa kwa mtu kujitenga nazo mbali na badala yake afuatilie mawaidha ya Qur-aan na Sunnah. Isipokuwa tu labda katika vita ili ziweze kusaidia kuleta motisha na jihaad katika njia ya Allaah (Ta´ala). Ni jambo zuri. Anaashiyd zikiambatana na dufu basi zinakuwa mbali zaidi na usawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ash-Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (01/134-135)
  • Imechapishwa: 05/06/2023