Swali: Wanayofanya baadhi ya watu kutuma karatasi ya Talaka kwa familia ya mke wake kunatosheleza kupita kwa Talaka?

Jibu: Ndio. Akiandika Talaka na kuituma kwake, Talaka inapita. Kwa kuwa kumtumia hii ni dalili ya kuwa kakusudia Talaka. Kwa kuwa wanachuoni wanasema, kule kuandika tu, haipiti Talaka mpaka mtu anuie. Na kumtumia karatasi, hii ni dalili ya kuwa kanuia. Talaka inakuwa imepita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10049
  • Imechapishwa: 03/03/2018