Swali 78: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na watoto wangapi?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na wavulana watatu:

1 – al-Qaasim, ambaye pia alikuwa akijulikana kama at-Twayyib na at-Twaahir. Alikuwa akiitwa kun-ya kwa jina hilo.

2 – ‘Abdullaah.

3 – Ibraahiym.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pia alikuwa na wasichana wanne:

1 – Faatwimah.

2 – Zaynab.

3 – Ruqayyah.

4 – Umm Kulthum.

Watoto wote wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwazaa na Khadiyjah, isipokuwa tu Ibraahiym. Wote walikufa kabla yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), isipokuwa tu Faatwimah.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 146
  • Imechapishwa: 13/11/2023