129. Waislamu wanapunguza masharubu na wanafuga ndevu zao

4 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jitofautisheni na washirikina! Punguzeni masharubu na zifugeni ndevu.”[1]

[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu ´Awaanah na al-Bayhaqiy kupitia kwa Naafiy´. Hata hivyo imekuja kwa Abu ´Awaanah:

”Jitofautisheni na waabudia moto.”

Hadiyth inatiliwa nguvu na nyingine aliyoipokea al-Bayhaqiy kupitia kwa Maymuun bin Mihraan, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitajiwa waabudia moto ambapo akasema: ”Hakika wao wanafuga masharubu yao na wananyoa ndevu zao. Jitofautisheni nao.”

Wasimulizi wake ni wenye kuaminika isipokuwa Abu Bakr Muhammad bin Ja´far al-Muzakkiy ambaye sijampata wasifu wake. Hata hivyo Ibn Hibbaan ameipokea kupitia njia nyingine na kwa ajili hiyo nimeitaja katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (2834). Vilevile inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Abu Hurayrah inayokuja:

”Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu na jitofautisheni na waabudia moto.”

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Hiyo ndio maana ya Hadiyth ya Ibn ´Umar. Walikuwa wakipunguza ndevu zao na wengine katika wao walikuwa wakizinyoa.” (Fath-ul-Baariy)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 184
  • Imechapishwa: 14/11/2023