Swali: Ni ipi hukumu ya kunyoa nywele za mikononi na miguuni kwa ajili ya kujipamba? 

Jibu: Sitambui ubaya wa jambo hilo. Hakuna ubaya kwa mwanamke kunyoa nywele za mikononi  na miguuni mwake. Sijui ubaya wa jambo hilo. Kuhusu nywele za usoni hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): 

“Amemlaani mwanamke anayechonga nyusi zake na mwanamke anayechongwa.” 

Maimamu wa lugha wamesema kuwa (النامصةni mwanamke ambaye anaondosha nywele za usoni mwake na nyusi pia. Hilo ndio jambo lililokatazwa. Lakini zikiota ndevu, masharubu, zikamea nywele kwenye mikono na miguu yake ni sawa akaziondosha. Hakuna ubaya katika kufanya hivo –  Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4489/حكم-ازالة-النساء-لشعر-الايدي-والارجل
  • Imechapishwa: 13/11/2023