Swali: Vipi kuhusu mavazi ya kuonyesha ndani? 

Jibu: Hapana, mavazi ya kuonyesha ndani hayajuzu. Mavazi ya kuonyesha ndani ni ya khatari yanaweza kuonyesha uchi. Lakini ikiwa ni mavazi ya kuonyesha ndani mikono jambo ni jepesi kidogo muda wa kuwa sehemu nyingine ya mwili imefunikwa vizuri. Ni lazima mavazi yawe yenye kusitiri na yanayopwaya. Kwa msemo mwingine mavazi yasiwe yenye kuonyesha rangi ya ngozi. Yafunike kitu hicho. Chini ya vazi hilo kuwepo vazi jengine jepesi kama vile flana na mfano wake. Kwa kifupi ni kwamba mavazi yenye kuonyesha ndani ni kama aliye uchi. Mavazi yenye kuonyesha ndani ni kama sampuli ya aliye uchi. Kwa hiyo mtu anapaswa kujihadhari na asilichukulie wepesi jambo hilo. 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4575/حكم-لبس-الملابس-الشفافة-امام-المحارم%C2%A0
  • Imechapishwa: 13/11/2023