128. Waislamu hawavai mavazi kama ya watawa

2 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nakutahadharisheni na nguo za watawa. Kwani hakika yule atakayezivaa, au akajifananisha nao, basi hatokamani na mimi.”[1]

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi nzuri, imekuja namna hiyo katika ”Fath-ul-Baariy”. Hata hivyo katika chapa hii nasema kuwa pengine Haafidhw Ibn Hajar anachomaanisha ni kuwa cheni ya wapokezi ni nzuri kupitia zingine. Hivi sasa nimepata mlolongo wa wapokezi wake na ikanibainikia kuwa ina kasoro kadhaa ambazo zinanilazimu kuidhoofisha. Kwa ajili hiyo Hadiyth hiyo hivi sasa inapatikana katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (3234).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 184
  • Imechapishwa: 13/11/2023