Mume kaniahidi kuanza kuswali baada ya ndoa ila hakutimiza ahadi yake

Swali: Miaka mitano ya kabla nimeolewa na mwanaume mmoja hivi, na kabla ya ndoa nimemuuliza kuhusu swalah akanambia kuwa haswali na akaniahidi kuwa ataanza kuswali baada ya ndoa – Allaah akitaka. Lakini kwa masikitiko makubwa, baada ya ndoa imedhihiri kuwa hatimizi ahadi yake na wala hatimizi swalah za faradhi isipokuwa swalah ya Ijumaa peke yake ndio anaswali msikitini. Na daima humuombea kwa kuwa mimi namcha Allaah. Na nimesikia kuwa haijuzu kuishi na mtu ambaye ni kafiri mwenye kuacha swalah. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Ndio, haijuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 01/02/2024