Swali: Yatosheleza kwa mwanamke kuswali nyumbani kwake kwa adhaana peke yake, au kwa adhaana na Iqaamah? Hali kadhalika mwanaume akichelewesha swalah yake na akaiswali nyumbani kwake, kinyume na wakati wake au katika wakati wake, inatosheleza kwake Iqaamah au ni lazima atoe adhaana na Iqaamah?

Jibu: Ama mwanaume inatosha kwake Iqaamah, kwa kuwa kishasikia adhaana. Wakati wa kuswali atakimu tu. Ama mwanamke, hana juu yake Iqaamah wala adhaana. Ni juu yake kuswali bila ya Iqaamah wala adhaana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 01/02/2024