Swali: Ni ipi hukumu ya kujitoa manii mchana wa Ramadhaan? Ni lipi linalomlazimu endapo alifamya hivo siku nyingi za Ramadhaan na hajalipa mpaka hivi sasa?

Jibu: Ikiwa anajitoa manii, kitendo hichi ni haramu katika Ramadhaan na miezi mingine. Ikiwa alimwaga, kitendo hichi kinaiharibu swawm yake. Kwa kuwa amejitoa matamanio yake kwa kufanya punyeto. Punyeto inaharibu swamw yake. Anapata dhambi. Ni lazima kwake kukimbilia kuleta tawbah. Ni lazima kwake kulipa. Ni wajibu vilevile kulisha kwa kila siku moja masikini kama tulivyotangulia kusema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 03/06/2017