Swali: Nilioa nami nilikuwa bado mdogo, na baada ya kuoa kwa takriban miezi kama mitatu nikwamwambia mke wangu mara nyingi: “Mimi sikutaki!”. Waambie wazazi wako kuwa mimi sikutaki”, pamoja na kuwa ni mke mwema. Na sasa sijui maneno niliyomwambia mke wangu huchukuliwa nimemtaliki au hapana? Kwa kuwa sikukusudia kumtaliki kwa kumwambia hivyo. Na ikiwa kama nimemtaliki, je nifunge nae ndoa upya kwa mara ya pili?

Jibu: Maneno haya haiwi talaka, uliyasema bila ya kukusudia hivyo, haiwi talaka. Maadamu hakunuwia talaka, si talaka. Bado ni mke wake.

Swali: Je, ana kafara yoyote kwa hilo?

Jibu: Hana juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 01/02/2024