Swali: Nimemuapia mke wangu Talaka kwenye mkanda na nikamtumia nao, na kusema: “Ni juu yangu talaka ikiwa sintoenda na nikachukua kiwango hichi kwa kaka yako, basi mimi nitakuwa nimekutaliki.” Na baada ya hapo nikasafiri kwenda Misri na sikufanya lolote kuhusiana na yamini hii. Naomba faida.

Jibu: Ikiwa kwa yamini hii, ulikusudia nafsi yako usifanye kitu hiki, au ulikusudia uweze kufanya kitu hiki. Ikiwa makusudio ni kuihimiza nafsi yako kufanya au kutofanya kitu, na makusudio haikuwa kufarakana nae na kumtaliki, hukumu ya hili ni hukumu ya yamini kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ama ikiwa ulikusudia kupita kwa talaka ikiwa utafanya au hutofanya, katika hali hii talaka inapita ikiwa hukufanya. Ikiwa kama ulikusudia kupita kwa talaka.