Kuoa mtoto wa mjomba na mama mdogo au mama mkubwa

Swali: Je, ni sahihi kwangu kufanya ndoa na msichana wa mama mdogo au hapana?

Jibu: Kufanya ndoa na msichana wa mama mdogo na mjomba, wote hawa inajuzu. Lililo la haramu ni kumuoa mama mdogo au shangazi mwenyewe. Ama msichana wa mama mdogo, msichana wa shangazi na msichana wa mjomba, hakuna ubaya wa hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 01/02/2024