Swali: Nilianza kupata ndoto nilipokuwa na umri wa miaka 13, na sikuswali wala kufunga ila nilipofikisha miaka 15, na hilo ni kutokana na ujinga wangu. Je, ni juu yangu kulipa swalah na swawm ya miaka miwili hii iliyopita au hapana?
Jibu: Mtu akibalaghe miaka kumi na tatu kwa kuteremsha manii, kisha akaacha swalah na swawm kwa ujinga, hana juu yake kulipa. Kwa kuwa kuacha swalah ni kufuru. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mtu aliyebaleghe kuacha swalah ni kufuru kubwa kwa wanachuoni wahakiki, na hii ndio Ijmaa´ ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Na linatolewa dalili hilo na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao [makafiri] ni swalah, atakayeiacha kakufuru.” (Hadiyth Swahiyh, kaipokea Imaam Ahmad na Ahl-us-Sunan)
Maneno yake tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha swalah.” (Kaipokea Muslim)
Tawbah inatosha, maadam katubu kwa Allaah tawbah ya kweli, inatosha na huna juu yako kulipa, si swawm wala swalah. Kwa kuwa aliyeritadi halipi kitu, na mwenye kuacha swalah anazingatiwa kuwa ni mwenye kuritadi kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yake kutubu kwa Allaah upya na wala asilipe kitu. Achunge jambo hili katika mustakabali, kwa kuleta tawbah ya kweli na kujilazimisha na ´amali njema.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
- Imechapishwa: 01/02/2024
Swali: Nilianza kupata ndoto nilipokuwa na umri wa miaka 13, na sikuswali wala kufunga ila nilipofikisha miaka 15, na hilo ni kutokana na ujinga wangu. Je, ni juu yangu kulipa swalah na swawm ya miaka miwili hii iliyopita au hapana?
Jibu: Mtu akibalaghe miaka kumi na tatu kwa kuteremsha manii, kisha akaacha swalah na swawm kwa ujinga, hana juu yake kulipa. Kwa kuwa kuacha swalah ni kufuru. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mtu aliyebaleghe kuacha swalah ni kufuru kubwa kwa wanachuoni wahakiki, na hii ndio Ijmaa´ ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Na linatolewa dalili hilo na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao [makafiri] ni swalah, atakayeiacha kakufuru.” (Hadiyth Swahiyh, kaipokea Imaam Ahmad na Ahl-us-Sunan)
Maneno yake tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha swalah.” (Kaipokea Muslim)
Tawbah inatosha, maadam katubu kwa Allaah tawbah ya kweli, inatosha na huna juu yako kulipa, si swawm wala swalah. Kwa kuwa aliyeritadi halipi kitu, na mwenye kuacha swalah anazingatiwa kuwa ni mwenye kuritadi kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yake kutubu kwa Allaah upya na wala asilipe kitu. Achunge jambo hili katika mustakabali, kwa kuleta tawbah ya kweli na kujilazimisha na ´amali njema.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
Imechapishwa: 01/02/2024
https://firqatunnajia.com/kulipa-swalah-alizoacha-mtu-utotoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)