Amefariki (Rahimahu Allaah) hali ya kuwa ni fakiri hana mali yoyote, lakini ana ujira na thawabu, na kaeneza elimu, Da´wah na imedhihiri dini ya Allaah (´Azza wa Jalla). Kama amevyosema Allaah (Jalla wa ´Alaa):’

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ

“Yeye Ndiye Aliyemtuma Mtume Wake kwa Uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu ya dini zote, japo washirikina watachukia.” (09:33)

Hii ndio Da´wah ya Shaykh kwa kifupi. Na hivi ndivyo vitabu na vijitabu vyake. Tutataja tunavyokumbuka. Kajaza ndani yake, hoja na dalili alizonazo. Na elimu pana aliyokuwa nayo. Na ufichuaji wake wa upotofu na shubuha. Vitabu vyake vimejaa haya. Kama mnavyoshuhudia wenyewe kwa kusoma “Kitaab-ut-Tawhiyd”. Katika Fiqh alikuwa katika madhehebu ya Imaam Ahmad bin Hanbal. Ama katika ´Aqiydah alikuwa katika ´Aqiydah ya Salaf-us-Swaalih; katika Maswahabah, Taabi´iyn, wafuasi wao na maimamu wanne. Hakuja na madhehebu mapya. Isipokuwa, alikuwa ni Hanbaliy Salafiy. Hanbaliy katika madhehebu, Salafiy katika ´Aqiydah. Alikuwa hasemi ila yale yale wanayosema maimamu wa kabla yake, na wala hafutu isipokuwa kwa yale yenye dalili ya wazi. Na hii ndio Manhaj ya maimamu (Rahimahu Allaah) wote. Imaam [Ibn ´Abdil-Wahhaab] hakuja na madhehebu ya kipekee. Yako wapi madhehebu yake ya kipekee kama wanavyodai?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=vns1tm7ddk4
  • Imechapishwa: 01/02/2024