Je, inafaa kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mtoto tumboni mwa mama yake?

Swali: Je, inafaa kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mtoto tumboni mwa mama yake?

Jibu: Inapendeza kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mtoto aliyeko tumboni kutokana na kitendo cha ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na wala si lazima. Kwa sababu ingefungamanishwa naye kabla ya kuonekana kwake basi zakaah ingefungamanishwa na vijusi vya wajane.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (3382)
  • Imechapishwa: 12/05/2022