Baba kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mwanae na wajukuu

Swali: Mimi ni mtu ninaishi na baba yangu nyumbani kwake na nimeoa na nina watoto. Je, inafaa kwa baba yangu kunitolea Zakaat-ul-Fitwr mimi na watoto wangu?

Jibu: Hapana neno baba yako akikutolea Zakaat-ul-Fitwr wewe, watoto wako na mke wako. Itasihi. Lakini bora ni wewe kujitolea mwenyewe na kwa wale walioko chini yako kwa sababu wewe ndiye umezungumzishwa jambo hilo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (19226)
  • Imechapishwa: 12/05/2022