Zakaat-ul-Fitwr ya mapacha waliozaliwa siku chache kabla ya ´iyd

Swali: Mke wangu alikuwa mjamzito katika mwezi wa Ramadhaan uliyobarikiwa na nikamtolea Zakaat-ul-Fitwr kipomoko kimoja kilichoko tumboni mwa mama yake. Siku chache kabla ya siku ya ´Iyd-ul-Fitwr mama alijifungua mapacha mawili kwa uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kuna kitu kinachonilazimu hivi sasa kwa vile nilimtolea Zakaat-ul-Fitwr kipomoko kimoja na sikukitolea kingine?

Jibu: Hakuna kinachokulazimu kwa kuacha kwako kukitolea Zakaat-ul-Fitwr kipomoko kingine.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/367) nr. (10816)
  • Imechapishwa: 12/05/2022