Zakaat-ul-Fitwr kwa mke ambaye ameenda kuwatembelea wazazi wake

Swali: Tumejua kuwa Zakaat-ul-Fitwr ni lazima kwa kila muislamu na anatakiwa kujitolea mwenyewe na kila ambaye analazimika kuwahudumia akiwemo mtoto, mke na mfanya kazi. Iwapo mke wa muislamu atasafiri kuwatembelea wazazi wake katika nchi nyingine na akakaa huko miezi miwili au zaidi mpaka ikafika siku ya ´Iyd-ul-Fitwr na yeye yuko kwa wazazi wake –  je, mume analazimika kumtolea Zakaat-ul-Fitwr au wazazi wake kwa sababu yuko kwao wakati wa kutolewa kwake?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivyotaja basi Zakaat-ul-Fitwr ya mke inamlazimu mume wake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (15767)
  • Imechapishwa: 12/05/2022