Zakaat-ul-Fitwr kwa ambaye amefunga Ramadhaan mji mwingine

Swali: Je, inafaa kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mke wangu kwa sababu mimi nimefunga Ramadhaan nikiwa katika mkoa wa mashariki na mke wangu akiwa kusini?

Jibu: Mtu hutoa Zakaat-ul-Fitwr yale maeneo alipo mtu. Hata hivyo itafaa ikiwa wakala wake au msimamizi wake atamtoela katika mji ambao yeye hayupo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/385) nr. (6829)
  • Imechapishwa: 12/05/2022