Swali 7344: Ni ipi hukumu ya maji ya mvua yanayokusanyika katika mabwawa yaliyotengenezwa? Kwa kuwa watu huyatumia kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa na ndogo na huyatumia kwa kuoga na kutawadha. Huenda watoto wakaogelea ndani yake na inawezekana wakakojoa humo, lakini hili ni jambo la uwezekano tu. Je, Hadiyth inayosema:
“Maji yanapokuwa zaidi ya Qullatayn[1], basi hayapati najisi.”
inahusu maji hayo?
Jibu: Asili ya maji ni kwamba ni twahara yenyewe na yenye kutwaharisha vingine, isipokuwa ikiwa rangi, ladha au harufu yake itabadilika kwa sababu ya najisi iliyotokea ndani yake.
[1] Takriban lita 300.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/73)
- Imechapishwa: 14/10/2026
Swali 7344: Ni ipi hukumu ya maji ya mvua yanayokusanyika katika mabwawa yaliyotengenezwa? Kwa kuwa watu huyatumia kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa na ndogo na huyatumia kwa kuoga na kutawadha. Huenda watoto wakaogelea ndani yake na inawezekana wakakojoa humo, lakini hili ni jambo la uwezekano tu. Je, Hadiyth inayosema:
“Maji yanapokuwa zaidi ya Qullatayn[1], basi hayapati najisi.”
inahusu maji hayo?
Jibu: Asili ya maji ni kwamba ni twahara yenyewe na yenye kutwaharisha vingine, isipokuwa ikiwa rangi, ladha au harufu yake itabadilika kwa sababu ya najisi iliyotokea ndani yake.
[1] Takriban lita 300.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/73)
Imechapishwa: 14/10/2026
https://firqatunnajia.com/wudhuu-kwa-maji-ya-mabwawa-ambayo-mtu-anahisi-yamekojolewa/