Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mu´aawiyah ni mjomba wa waumini. Alikuwa ni mwandishi wa Wahy wa Allaah na alikuwa ni mmoja wa viongozi wa waislamu (Radhiya Allaahu ´anh).

MAELEZO

Ni kiongozi wa waumini Mu´aawiyah bin Abiy Sufyaan Swakhr bin Harb. Alizaliwa miaka mitano kabla ya kutumilizwa na akasilimu mwaka wa Ufunguzi. Kuna maoni vilevile yanayosema kuwa alisilimu baada ya Hudaybiyah na akaficha Uislamu wake. ´Umar alimtawalisha Shaam na akaendelea katika hilo. Akaitwa kiongozi baada ya hukumu mbili mwaka wa 37 baada ya kuhajiri. Watu walikusanyika kwake baada ya al-Hasan bin ´Aliy kujiuzulu mwaka wa 41 baada ya kuhajiri. Alikuwa akimwandikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anahesabika ni miongoni mwa waandishi wa Wahy. Alikufa Rajab mwaka wa 60 baada ya kuhajiri akiwa na miaka 78.

Mtunzi wa kitabu amemtaja na akamsifu kwa ajili ya kuwaraddi Raafidhwah ambao wanamtukana na kumchafua. Amemwita mjomba wa waumini kwa sababu yeye ni kaka yake na Habiybah ambaye ni mmoja katika mama wa waumini. Shaykh-ul-Islaam ametaja katika “Minhaaj-us-Sunnah” (02/199) makinzano ya wanazuoni na kama inafaa kuwaita kaka za wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wajomba wa waumini au hapana?

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 17/12/2022