Swali: Mtu huyu anatafuta riziki kwa njia ya kutangaza katika baadhi ya majarida au mitaa ya kwamba yuko na mabasi na anawabeba baadhi ya waalimu wa kike nje ya ar-Riyaadh ambapo kuna mwendo wa karibu 200 km na wakati huo anakuwa pamoja na mke au mahram wake na wanawake sita au watano.

Jibu: Kilicho cha lazima ni wanawake hao wasisafiri isipokuwa wawe pamoja na mahram. Hili ndio salama zaidi. Baadhi ya wanazuoni wanaruhusu jambo hili inapohitajika na kukiwa na amani. Lakini udhahiri wa Sunnah ni kutokufaa isipokuwa akiwa na mahram. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja na mahram.”

Swali: Lakini wanasema kuwa hiyo ndio riziki yake anayoichukua kutoka kwa waalimu hao wa kike. Je, aendelee?

Jibu: Salama zaidi ni yeye kuiacha na atafute kazi nyingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22222/حكم-سفر-نساء-مع-ساىق-ومحرم-له
  • Imechapishwa: 17/12/2022