Inafaa kufanya biashara na washirikina

Swali: ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa na nguo yake ya ngao ya vita imewekwa rehani kwa myahudi.”

Jibu: Inaonyesha kufaa kufanya biashara na washirikina ambapo mtu akanunua kutoka kwao na akawauzia. Hapana vibaya kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinunua kutoka kwa mayahudi na akaweka kwao nguo yake ya ngao ya vita.

Swali: Vipi wasiokuwa mayahudi?

Jibu: Ni mamoja mayahudi, manaswara na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22223/ما-هدي-النبي-ﷺ-في-معاملة-المشركين
  • Imechapishwa: 17/12/2022