Kuhusu uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Abu Twaalib ili awe katika adhabu ndogo ya Moto na huku amevaa viatu viwili ambavyo vinachemsha ubongo wake – na huyu ndiye mtu wa Motoni mwenye adhabu ya chini kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kama isingelikuwa mimi basi angelikuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni.”

Ameipokea Muslim.

Uombezi huu ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa ami yake Abu Twaalib peke yake. Hilo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kutokana na ile kazi aliyofanya ya kumnusuru na kumtetea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyokuja nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 130-131
  • Imechapishwa: 06/12/2022