87. Pepo kwa ajili ya waumini na Moto kwa ajili ya makafiri

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Pepo na Moto vimeumbwa na havitotoweka. Pepo ni makazi ya wapenzi Wake na Moto ni adhabu ya maadui Wake. Watu wa Peponi watadumu humo milele

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ

”Hakika wahalifu wamo kwenye adhabu ya [Moto wa] Jahannam watadumu milele. Hawatopumzishwa nayo nao humo watakata tamaa.”[1]

MAELEZO

Pepo maana yake kilugha ni bustani yenye miti mingi. Pepo maana yake katika Shari´ah ni makazi ambayo Allaah ameyaandaa huko Aakhirah kwa ajili ya wenye kumcha.

Moto maana yake kilugha inatambulika. Moto maana yake katika Shari´ah ni makazi ambayo Allaah ameyaandaa huko Aakhirah kwa ajili ya makafiri.

Pepo na Moto tayari vimekwishaumbwa hivi sasa. Amesema (Ta´ala) kuhusu Pepo:

أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[2]

Amesema kuhusu Moto:

أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

”Umeandaliwa kwa makafiri.”[3]

Maana ya kuandaliwa ni kutayarishwa.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati aliposwali swalah ya kupatwa kwa jua:

“Mimi nimeona Pepo na nikachukua kole la zabibu. Kama ningechukua makole mengi basi mgeyala muda wa kubakia dunia. Na nimeona Moto pia na sijapata kuona kitu cha kutisha sana kuliko hiyo.”[4]

Kuna maafikiano juu yake.

[1] 43:74-75

[2] 03:133

[3] 02:24

[4] al-Bukhaariy (1052) na Muslim (907, 17).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 131
  • Imechapishwa: 05/12/2022