Kuwa na utambuzi juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni miongoni mwa mambo ya wajibu ya dini na ni katika misingi ya Uislamu. Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba ni wajibu juu yetu kujifunza masuala manne:

Suala la kwanza: Ujuzi wa kumtambua Allaah, Mtume Wake na dini ya Uislamu kwa dalili.”[1]

Kama ambavyo inakupasa kumtambua Allaah basi vivyo hivyo ni lazima kuwa na utambuzi kuhusu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na dini ya Uislamu kwa dalili. Hii ndio misingi mitatu ambayo maiti anaulizwa nayo anapolazwa ndani ya kaburi lake.

[1] Thaalathat-ul-Usuwl.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 57
  • Imechapishwa: 05/12/2022