Uombezi huu unapingwa na Mu´tazilah na Khawaarij kutokana na ´Aqiydah yao kwamba watenda madhambi makubwa watadumishwa Motoni milele. Kwa hivyo wanaona kuwa hautowafaa uombezi. Tunawaraddi kwa yafuatayo:

1 – Hilo linaenda kinyume na Hadiyth tele zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Linaenda kinyume na maafikiano ya Salaf.

Uombezi una sharti mbili:

1 – Idhini ya Allaah kwa uombezi. Amesema (Ta´ala):

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake?”[1]

2 – Allaah ampe idhini mwenye kuombea na mwenye kuombewa. Amesema (Ta´ala):

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ

“Na wala hawamuombei uombezi yeyote yule isipokuwa yule Anayemridhia.”[2]

Kuhusu kafiri hana uombezi wowote. Amesema (Ta´ala):

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi.”[3]

Bi maana tutakadiria mtu kuwaombea basi hautowafaa kitu uombezi wao.

[1] 02:255

[2] 21:28

[3] 74:48

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 130
  • Imechapishwa: 06/12/2022