2 – Uombezi ulioenea. Ni uombezi kwa wale waumini waliotenda madhambi makubwa walioingia Motoni watoke humo baada ya kuunguzwa na wakawa majivu na mkaa. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuhusu watu wa Motoni ambao ndio watakaa milele hawatokufa ndani yake na wala hawatopata uhai. Lakini kuna watu – au kama alivosema – ambao Moto utawapata kwa sababu ya madhambi yao” au alisema “kwa sababu ya makosa yao ambapo atawafisha kidogo mpaka wakishakuwa majivu ndio watapewa idhini ya kuombewa.”[1]

Hadiyth hii ameipokea Ahmad.

Ibn Kathiyr amesema katika “an-Nihaayah” (02/204):

“Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim na hawakuipokea kwa muundo huu.”

Uombezi huu utakuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mitume wengine, Malaika na waumini. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ndani yake imetajwa:

“Allaah (Ta´ala) atasema: “Malaika wameombea, Mitume wameombea, waumini wameombea na hakuna aliyebaki isipokuwa Mwingi wa rehema wa kurehemu. Ndipo atashika mshiko katika Moto na awatoe watu ambao hawajapapo kufanya kheri hata siku moja na wameshakuwa ni majivu.”

Kuna maafikiano juu yake.

[1] Ahmad katika ”al-Musnad” yake (03/94).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 05/12/2022