Swali: Nimesoma kwamba haijuzu kuingia chooni ukiwa na msahafu Mtukufu. Je, hukumu hii inahusu pia kanda za kurekodi zilizoandikwa Qur-aan? Je, inajuzu kuingia humo ukiwa na vitabu vya Kiislamu au visivyo vya Kiislamu ambavyo ndani yake kuna jina la Allaah (Ta´ala)?
Jibu: Haijuzu kuingia chooni ukiwa na msahafu Mtukufu. Ama kanda na mfano wake zilizoandikwa Qur-aan na vilevile vitabu vya kielimu, ni mamoja vilivyoandikwa au visivyoandikwa, ambavyo ndani yake kuna utajo wa Allaah, basi inachukiza kuingia navyo ikiwa hakuna haja. Ama ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, basi hakuna machukizo.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/95)
- Imechapishwa: 14/10/2026
Swali: Nimesoma kwamba haijuzu kuingia chooni ukiwa na msahafu Mtukufu. Je, hukumu hii inahusu pia kanda za kurekodi zilizoandikwa Qur-aan? Je, inajuzu kuingia humo ukiwa na vitabu vya Kiislamu au visivyo vya Kiislamu ambavyo ndani yake kuna jina la Allaah (Ta´ala)?
Jibu: Haijuzu kuingia chooni ukiwa na msahafu Mtukufu. Ama kanda na mfano wake zilizoandikwa Qur-aan na vilevile vitabu vya kielimu, ni mamoja vilivyoandikwa au visivyoandikwa, ambavyo ndani yake kuna utajo wa Allaah, basi inachukiza kuingia navyo ikiwa hakuna haja. Ama ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, basi hakuna machukizo.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/95)
Imechapishwa: 14/10/2026
https://firqatunnajia.com/vitabu-vya-kielimu-chooni/