Swali 4448: Je, inajuzu kutamka Bismillaah, Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr ndani ya bafu wakati wa kutawadha au haijuzu?

Jibu: Inachukiza kumtaja Allaah (Ta´ala) kwa kutamka kwa sauti ndani ya bafu ambalo mtu hutekeleza haja, kwa kutukuza jina Lake na kuliheshimu. Lakini imesuniwa kwake kutamka Bismillaah mwanzoni mwa wudhuu´, kwa sababu ni wajibu pamoja na Dhikr kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/94)
  • Imechapishwa: 14/10/2026