Utumiaji wa maji najisi yaliyosafishwa

Swali: Katika siku hizi, maji yanayotiririka kwenye mifereji ya majitaka hukusanywa pamoja na najisi katika baadhi ya nchi, kisha husafishwa tena ili yarudi majumbani mara nyingine. Je, kile kiini cha najisi kimekuwa twahara katika maji hayo?

Jibu: Asili ya maji ni twahara. Hayo uliyoyataja kuhusu maji ya majitaka yamekuwa najisi kwa sababu yamechanganyika na mkojo, kinyesi na mfano wa hivyo. Ikiwa yatasafishwa tena na kuondolewa najisi na ikaondoka harufu ya najisi, ladha yake na rangi yake, basi yanakuwa twahara. Vinginevyo yanakuwa najisi kwa sababu ya athari na dalili za najisi zilizobaki ndani yake.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/82)
  • Imechapishwa: 14/10/2026