Swali: Je, inajuzu kutawadha kwa ajili ya swalah kwa kutumia maji ya bahari? Ikiwa niko kando ya bahari na nina maji matamu yanayopatikana, je, nitawadhe kwa kutumia maji matamu au maji ya bahari? Kwa kuwa inasemekana kwamba haijuzu kutawadha kwa kutumia maji ya bahari isipokuwa wakati wa dharurah. Baadhi ya watu wanasema haijuzu kutawadha kwa kutumia maji hayo.
Jibu: Inajuzu kwako kutawadha kwa kutumia maji ya bahari kwa mujibu wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Maji yake ni twahara na mnyama wake aliyekufa ni halali.”[1]
Hakuna tofauti katika hilo, ni mamoja ikiwa una maji matamu ya kutawadha nayo au huna.
[1] Ahmad (02/237), Abu Daawuud (392) an-Nasaa´iy (01/44) na wengineo.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/74-75)
- Imechapishwa: 14/10/2026
Swali: Je, inajuzu kutawadha kwa ajili ya swalah kwa kutumia maji ya bahari? Ikiwa niko kando ya bahari na nina maji matamu yanayopatikana, je, nitawadhe kwa kutumia maji matamu au maji ya bahari? Kwa kuwa inasemekana kwamba haijuzu kutawadha kwa kutumia maji ya bahari isipokuwa wakati wa dharurah. Baadhi ya watu wanasema haijuzu kutawadha kwa kutumia maji hayo.
Jibu: Inajuzu kwako kutawadha kwa kutumia maji ya bahari kwa mujibu wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Maji yake ni twahara na mnyama wake aliyekufa ni halali.”[1]
Hakuna tofauti katika hilo, ni mamoja ikiwa una maji matamu ya kutawadha nayo au huna.
[1] Ahmad (02/237), Abu Daawuud (392) an-Nasaa´iy (01/44) na wengineo.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/74-75)
Imechapishwa: 14/10/2026
https://firqatunnajia.com/kutawadha-kwa-maji-ya-bahari/