Swali: Sisi tuko na msikiti wenye makaburi mawili ndani ya ua. Je, inajuzu kuyahamisha au yabaki mahali yalipo?

Jibu: Ikiwa katika msikiti kuna makaburi mawili ndani ya uzio wake, basi kama makaburi hayo yaliwekwa ndani ya msikiti baada ya kujengwa kwake, ni wajibu kuyaondoa. Yafukuliwe na mabaki yao yahamishiwe kwenye makaburi ya jumla ya waislamu na hairuhusiwi kabisa kubaki kwao ndani ya msikiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani mayahudi na manaswara. Wamefanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia.”

“Zindukeni! Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao na watu wema wao kuwa ni mahali pa kuswalia. Zindukeni! Msifanye makaburi kuwa mahali pa kuswalia, kwani hakika mimi nawatahadhalisha na hilo.”

Wanazuoni wameeleza wazi kwamba haijuzu kuzika ndani ya misikiti na kwamba ikiwa mtu amezikwa humo basi ni lazima afukuliwe na ahamishwe kwenda kwenye makaburi ya waislamu.

Mwanafuzni: Ninaweza kuswali ndani ya msikiti huu iwapo nitapita karibu na msikiti nao?

Ibn Baaz: Hapana, hapana. Usiswali na ndani yake kuna kaburi. Usiswali pamoja nao.

Mwanafunzi: Vipi ikiwa makaburi yamekuja kabla ya msikiti?

Ibn Baaz: Msikiti utabomolewa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3271/حكم-نبش-القبور-التي-توجد-داخل-سور-المسجد-والصلاة-فيه
  • Imechapishwa: 12/10/2026