Swali: Ami yangu alioa wanawake wawili ambapo mwanamke mmoja alizaa mtoto wa kiume na mwingine akazaa mtoto wa kike. Mimi nilinyonya kutoka kwa mama wa yule binti. Je, inajuzu mimi kumuoa binti wa yule mtoto wa kiume ambaye alizaliwa na mwanamke ambaye sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Ikiwa umenyonya kutoka kwa mama wa yule binti, basi unakuwa mtoto wa huyo mwanaume. Ikiwa unyonyeshaji ulikuwa kamili kusikopungua mara tano, basi unakuwa mtoto wake na ndugu wa watoto wake wote na mjomba kwa watoto wao. Hivyo basi hairuhusiwi kwako kufanya hivyo. Ukinyonya kutoka kwa mmoja wa mkewe mtu, wakeze mtu, basi unakuwa mtoto wake. Hapo ni pale ambapo unyonyeshaji ni mara zisizopungua tano na ikiwa ni ndani ya miaka miwili, basi unakuwa mtoto wake na mjomba kwa watoto wake wote, kwa wake zake wote na mjomba kwa wasichana zake pia.
Swali: Je, siwi mtoto wake ikiwa sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Lakini yeye amenyonyesha, ikiwa hakunyonya hakuna haja.
Swali: Je, inajuzu mimi kumuoa binti wa yule mtoto wa kiume ambaye alizaliwa na mwanamke ambaye sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Anaoa binti wa ndugu yake. Huyo ni binti wa ndugu yako, hapana, huyo ni binti wa ndugu yako. Kwa sababu wewe ni ndugu wa watoto wake wote. Kwa hivyo wasichana wa watoto wake ni wasichana wa ndugu yako na wewe ni mjomba wao. Kwa hivyo usimuoe.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3264/حكم-الزواج-بابنة-ابن-العم-الذي-رضعت-من-زوجة-ابيه
- Imechapishwa: 12/10/2026
Swali: Ami yangu alioa wanawake wawili ambapo mwanamke mmoja alizaa mtoto wa kiume na mwingine akazaa mtoto wa kike. Mimi nilinyonya kutoka kwa mama wa yule binti. Je, inajuzu mimi kumuoa binti wa yule mtoto wa kiume ambaye alizaliwa na mwanamke ambaye sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Ikiwa umenyonya kutoka kwa mama wa yule binti, basi unakuwa mtoto wa huyo mwanaume. Ikiwa unyonyeshaji ulikuwa kamili kusikopungua mara tano, basi unakuwa mtoto wake na ndugu wa watoto wake wote na mjomba kwa watoto wao. Hivyo basi hairuhusiwi kwako kufanya hivyo. Ukinyonya kutoka kwa mmoja wa mkewe mtu, wakeze mtu, basi unakuwa mtoto wake. Hapo ni pale ambapo unyonyeshaji ni mara zisizopungua tano na ikiwa ni ndani ya miaka miwili, basi unakuwa mtoto wake na mjomba kwa watoto wake wote, kwa wake zake wote na mjomba kwa wasichana zake pia.
Swali: Je, siwi mtoto wake ikiwa sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Lakini yeye amenyonyesha, ikiwa hakunyonya hakuna haja.
Swali: Je, inajuzu mimi kumuoa binti wa yule mtoto wa kiume ambaye alizaliwa na mwanamke ambaye sikunyonya kutoka kwake?
Jibu: Anaoa binti wa ndugu yake. Huyo ni binti wa ndugu yako, hapana, huyo ni binti wa ndugu yako. Kwa sababu wewe ni ndugu wa watoto wake wote. Kwa hivyo wasichana wa watoto wake ni wasichana wa ndugu yako na wewe ni mjomba wao. Kwa hivyo usimuoe.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3264/حكم-الزواج-بابنة-ابن-العم-الذي-رضعت-من-زوجة-ابيه
Imechapishwa: 12/10/2026
https://firqatunnajia.com/hukumu-ya-kumuoa-msichana-wa-binamu-aliyenyonyeshwa-na-mke-wa-baba-yake/