Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu ambazo hazitawaliwi kwa Shari´ah ya Allaah na watawala wake wanawapendelea maadui wa Allaah miongoni mwa makafiri na wapagani, vijana wa Kiislamu huangukia katika mshangao na wasiwasi, pamoja na uchache wa elimu na wingi wa wanazuoni wabaya, jambo linalowafanya vijana kuwa kati ya kupindukia kwa kuwakufurisha watawala na kutangaza jihaad dhidi yao. Baadhi yao wanaona ulazima wa elimu na kutafuta elimu ya Kishari´ah kwanza, kisha kuwalingania watu kwa Allaah kwa ujuzi, kwa hekima na mawaidha mazuri. Mara nyingi hutokea makinzano baina ya makundi mawili haya na kubadilishana tuhuma baina ya pande mbili. Tunaomba kutoka kwenu nasaha kwa hawa na hawa? Ni ipi njia sahihi kwa vijana hawa ili kuokoka na fitina hizi na kujisafisha mbele ya Allaah siku ya kukutana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: Nasaha kwa vijana hawa na wengineo miongoni mwa watu wazima na wazee kwamba wasitangulize jambo lolote isipokuwa kwa ujuzi na elimu na kwamba wajifunze dini kabla ya kila kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri, basi humfanya ufahamu katika dini.”
Kwa hiyo kufanya haraka na kutoa hukumu juu ya mambo bila elimu na bila ujuzi, bali kwa msukumo tu wa jihaad, msukumo wa wivu kwa ajili ya Allaah, mapenzi ya dini, kupenda kuidhihirisha haki au kupenda kuondoa maasi, hayo hayatoshi. Lazima kuwe na elimu, ujuzi na ufahamu wa dini. Aidha ni lazima kushauriana na wanazuoni wa kweli wenye ujuzi na uelewa, wanaojulikana kwa wivu wa Kiislamu na elimu ya Kishari´ah na ujuzi katika dini na kutojiharakisha katika jambo lolote. Ajifunze dini na ashikamane na viongozi wake katika mambo ya haki.
Ama mapinduzi hayaleti kheri. Mapinduzi hayaleti kheri isipokuwa kutoka kwa dola ya Kiislamu yenye nguvu inayoweza kupambana inapodhihiri ukafiri waziwazi, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama watu binafsi wakisimama, kwa kawaida huharibu wala hawatengenezi. Mara nyingi wakisimama na kuanzisha mambo hayo, husababisha kusimamishwa kwa ulinganizi, kufungwa kwa wanafunzi, kudhuriwa kwa wanafunzi na kusimamishwa kwa ulinganizi na elimu. Basi harakati hizi na mapinduzi hayaleti kheri. Bali kinacholeta kheri ni kujifunza, kufahamu dini, kulingania kwa Allaah, kuwapa nasaha watawala na kushirikiana nao katika mema na kuacha maovu. Kama ilivyokuja katika Hadiyth:
“Yeyote atakayeona kwa kiongozi wake jambo analolichukia katika maasi ya Allaah, basi achukie yale anayoyafanya ya maasi ya Allaah na wala asiondoe mkono wake katika utiifu.”
”Yeyoye atakayetoa mkono wake katika utiifu na akafa, basi atakufa kifo cha kipindi kabla ya kuja Uislamu.”
Maswahabah walimpa kiapo juu ya kutopinga uongozi kwa wenye mamlaka:
”… isipokuwa watapoona ukafiri wa wazi wenye dalili kutoka kwa Allaah.”
Kwa hiyo jambo hili linahitaji elimu, ujuzi na nguvu ya kuweza kuondoa dola yenye ukafiri waziwazi na kusimamisha dola ya Kiislamu. Ama watu binafsi wanaofanya uharibifu ardhini na kuwaua watu bila haki na bila elimu, hao huleta madhara makubwa, huharibu sana na husimamisha ulingano na elimu. Matokeo yake huwa mabaya kwa walinganizi, wenye kumtakasia imani, waalimu na waongozaji. Basi wajibu ni huu: kujifunza, kufahamu dini, kuwa na uelewa, kushirikiana na dola iliyopo katika yale yanayomridhisha Allaah katika kusimamisha haki na kuondoa batili na kuwapa nasaha ili wasimamishe mema na waache maovu. Kufanyika kwa kuelimisha vijana, kuwaongoza kwenye kheri na kuwafundisha ili waifahamu dini ya Allaah, watambue haki na waijue batili, kisha waitumie kwa nafsi zao na wawafundishe familia zao, ndugu zao na majirani zao na wanaohusiana nao, mpaka waifahamu dini. Watu wakifahamu dini na kuwa na uelewa, basi dola itanyenyekea katika kutekeleza amri ya Allaah juu yao na kuacha yale yanayokwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3236/كيفية-التعامل-مع-الحكام-الذين-لا-يحكمون-بشرع-الله
- Imechapishwa: 18/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3236/كيفية-التعامل-مع-الحكام-الذين-لا-يحكمون-بشرع-الله
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/tunatakiwa-kuwa-na-msimamo-gani-kwa-watawala-wasiohukumu-kwa-shariah/