Swali: Ni ipi tofauti kati ya amri ya makadirio na Kishari´ah na kati ya utashi na matakawa ya Kishari´ah na ya makadirio?
Jibu: Tofauti kati yao ni kwamba hukusanyika kwa mtiifu na hutofautiana kwa mtenda dhambi na kafiri. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ana matakwa aina mbili: makadirio na ya Kishari´ah. Matakwa ya makadirio ni yale yaliyotangulia katika ujuzi Wake na kinachotakiwa humo lazima kitokee. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ
”Hakika si venginevyo amri Yake anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa.”[1]
Matakwa ya makadirio ni yenye kutekelezeka. Amesema (Ta´ala):
فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ
“Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza, humfungulia kifua chake kwa Uislamu na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye uzito kana kwamba anapanda kwa tabu mbinguni.”[2]
Kuna matakwa ya Kishari´ah, kama alivyosema (Ta´ala):
يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ
”Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu.”[3]
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا
“Allaah anataka kukukhafifishieni, kwani mtu ameumbwa dhaifu.”[4]
Haya ni matakwa Kishari´ah; ametaka wepesi na amewaamrisha waja Wake yale yenye kuwafaa. Lakini inaweza kutokea kwa baadhi ya watu na wengine isitokee. Anaweza kuamrishwa mtu kuswali, kufunga na kumuabudu Allaah peke Yake, lakini baadhi huswali na kufunga na kumuabudu Allaah, na wengine hukufuru – nao ndio wengi. Haya ni matakwa ya Kishari´ah.
Kwa hiyo mtiifu mwenye kumpwekesha kumekusanyika kwake utashi aina mbili; amekubaliana na matakwa ya kilimwengu, na pia amekubaliana na mipango ya Kishari´ah kwa kumtii Allaah na kumpwekesha. Ama muasi amekubaliana na matakwa ya kilimwengu, lakini amepingana na matakwa ya Kishari´ah na amri ya Kishari´ah. Vivyo hivyo kafiri.
[1] 36:82
[2] 06:125
[3] 02:185
[4] 04:28
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3232/الفرق-بين-الارادة-الكونية-القدرية-والارادة-الدينية-الشرعية
- Imechapishwa: 18/10/2026
Swali: Ni ipi tofauti kati ya amri ya makadirio na Kishari´ah na kati ya utashi na matakawa ya Kishari´ah na ya makadirio?
Jibu: Tofauti kati yao ni kwamba hukusanyika kwa mtiifu na hutofautiana kwa mtenda dhambi na kafiri. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ana matakwa aina mbili: makadirio na ya Kishari´ah. Matakwa ya makadirio ni yale yaliyotangulia katika ujuzi Wake na kinachotakiwa humo lazima kitokee. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ
”Hakika si venginevyo amri Yake anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa.”[1]
Matakwa ya makadirio ni yenye kutekelezeka. Amesema (Ta´ala):
فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ
“Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza, humfungulia kifua chake kwa Uislamu na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye uzito kana kwamba anapanda kwa tabu mbinguni.”[2]
Kuna matakwa ya Kishari´ah, kama alivyosema (Ta´ala):
يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ
”Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu.”[3]
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا
“Allaah anataka kukukhafifishieni, kwani mtu ameumbwa dhaifu.”[4]
Haya ni matakwa Kishari´ah; ametaka wepesi na amewaamrisha waja Wake yale yenye kuwafaa. Lakini inaweza kutokea kwa baadhi ya watu na wengine isitokee. Anaweza kuamrishwa mtu kuswali, kufunga na kumuabudu Allaah peke Yake, lakini baadhi huswali na kufunga na kumuabudu Allaah, na wengine hukufuru – nao ndio wengi. Haya ni matakwa ya Kishari´ah.
Kwa hiyo mtiifu mwenye kumpwekesha kumekusanyika kwake utashi aina mbili; amekubaliana na matakwa ya kilimwengu, na pia amekubaliana na mipango ya Kishari´ah kwa kumtii Allaah na kumpwekesha. Ama muasi amekubaliana na matakwa ya kilimwengu, lakini amepingana na matakwa ya Kishari´ah na amri ya Kishari´ah. Vivyo hivyo kafiri.
[1] 36:82
[2] 06:125
[3] 02:185
[4] 04:28
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3232/الفرق-بين-الارادة-الكونية-القدرية-والارادة-الدينية-الشرعية
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/tofauti-kati-ya-matakwa-ya-kilimwengu-na-matakwa-ya-kidini/