Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

70 – Abu Sa´iyd al-Kudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرةٌ، وإنَّ اللهَ مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا فَيَنْظُرَ كَيفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاء؛ فإنَّ أَوَّلَ فِتْنَةِ بَنِي إسرائيلَ كَانَتْ في النِّسَاءِ))

“Hakika dunia ni kijani kibichi. Hakika Allaah amekutawalisheni humo ili Atazame nini mtachofanya. Hivyo basi, iogopeni dunia na waogopeni wanawake. Hakika mtihani wa kwanza kwa wana wa israaiyl ilikuwa ni kwa wanawake.”[1]

Kuwaogopa wanawake ina maana ya kutahadhari nao. Hili linahusu kutahadhari na mwanamke katika vitimbi vyake na mume wake na pia wanawake wengine na fitina zao. Ndio maana akasema:

“Hakika mtihani wa kwanza kwa wana wa israaiyl ilikuwa ni kwa wanawake.”

Walifitinisha na wanawake. Hivyo wakapotea wao na kuwapoteza wengine. Ndio maana tunaona maadui zetu na maadui wa Uislamu ambayo ndio Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall) wamekazia juu ya suala la mwanamke, kuvaa vibaya, kuchanganyika na wanaume na kushirikiana na wanaume kazini. Wanachotaka ni watu wafikie kuwa kama punda. Wanataka kusiwe jengine watachojali isipokuwa matumbo yao na tupu zao. Wanachotaka mwanamke awe kama vile vidude vya kuchezea na picha. Watu wasitilie muhimu jengine isipokuwa fomu ya mwanamke; namna watakavyompamba, watakavyompodoa, mambo ya kumfanya akaonekana mzuri, nywele za bandia, vitu vya kutia na kupaka kwenye ngozi ya mwili, miguu, mikono, uso na mengineyo. Wanachotaka hamu kubwa ya wanawakeawe kama picha ya plastiki. Hajali ´ibaadah wala watoto.

Maadui zetu ambao ni maadui vilevile wa Allaah, Shari´ah ya Allaah na maadui wa hayaa wanataka kumpachika mwanamke kwenye kazi za wanaume ili wageuke kuwa kama mazuzu na kuwafanya vijana wajazane kwenye masoko na wasiwe na kazi nyingine, jambo ambalo linapelekea katika shari na mtihani ulio mkubwa. Ujana, faragha na nyimbo ni miongoni mwa ufisadi ulio mkubwa. Imesemwa:

Hakika ya ujana, faragha na nyimbo

ndio kuharibika kulio kukubwa kwa mtu

Leo wanataka kuwatia mtegoni wanawake kwa kazi za wanaume kisha wanawaita vijana. Wanafanya hivi ili vijana wao waharibike na wanawake pia waharibike. Mnajua ni nini kinachotokea? Inapelekea wao kufanya kazi pamoja na wanaume na hivyo kunapatikana uharibifu wa mchanganyiko, uzinzi na uchafu. Haijalishi kitu sawa ikiwa ni uzinzi wa macho, ulimi, mkono, tupu na mengineyo. Yote hayo yanawezekana ikiwa mwanamke anafanya kazi pamojana mwanaume.

Miji mingi ambayo wanaume wanafanya kazi na wanawake kunapatikana uchafu mwingi. Mwanamke akishaanza kufanya kazi hukosekana nyumbani kwake na mume pia humkosa. Akishaajiriwa kazini nyumba itahitaji mfanyakazi, jambo ambalo linapelekea kuleta wanawake wa ulimwenguni mzima kutoka kila pande, dini na tabia ya kila sampuli. Huletwa wafanyakazi wanawake hata wasiokuwa waislamu na tabia mbovu. Tunaleta wanawake ili wawe wafanyakazi majumbani na kuwaacha wanawake zetu wakafanyakazi sehemu za wanaume wenzetu. Tunawanyima kazi wanaume wenzetu na kuwapa kazi wanawake.

Madhara mengine yanayopatikana ni familia kutengana. Mtoto anapokuwa na hakuna mbele yake isipokuwa mfanyakazi humsahau mama na baba yake. Mtoto anakosa kule kufungamana nao, jambo ambalo hupelekea majumba kuharibika na kupatikana mpasuko. Katika hilo kuna uharibifu mkubwa unaopatikana unaojua Allaah pekee.

[1] Muslim (2742)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/525-526)
  • Imechapishwa: 29/06/2023