Hizi ni Hadiyth aina nne na watu wamezifasiri kwa njia nne:

1 – Kundi la kwanza linalosema kuwa ni kufuru ya neema.

2 – Kundi la pili linalosema kwamba inahusiana na matishio na kuogopesha.

3 – Kundi la tatu linalosema kuwa zinakusudia kufuru ya kuritadi.

4 – Kundi la nne wanazirudisha zote.

Kutokana na kasoro na uharibifu wa tafsiri zote hizi, sisi tunazirudisha na hatuzikubali.

Kuhusu tafsiri ya kundi la kwanza, hatujui kuwa lina msingi wowote katika lugha ya kiarabu. Kwa mujibu wa waarabu hawatambui kukufuru neema isipokuwa pale mtu anapokanusha neema za Allaah. Mfano wake ni kama mtu anayejiita kuwa ni masikini wa kupindukia ilihali Allaah amemtajirisha, au kwamba ni mgonjwa ilihali Allaah amempa uzima. Kunaingia pia mtu kuficha mazuri yake na kueneza misiba yake. Haya ndio waarabu huita kuwa ni kufuru, pasi na kujali uhusiano huo ni kati ya Allaah na mtu au kati ya watu wao kwa wato pindi wanapokanusha wema unaotendeka kati yao. Kinachotilia nguvu hilo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia wanawake:

”Hakika nyinyi mnakithirisha laana na mnamkufuru mume. Hilo pale anapoghadhibika mmoja wenu basi husema: ”Sijapatapo kamwe kuona kheri kwako.”[1]

Huku ndio kukufuru neema.

[1] al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 29/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy