4 – Madhambi yanayoitwa shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kikubwa ninachokhofia juu ya ummah wangu ni shirki ndogo.” Kukasemwa: “Ee Mtume wa Allaah! Ni ipi shirki ndogo?” Akasema: “Kujionyesha.”[1]

“Kuamini mkosi wa ndege ni shirki. Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa anahisi kitu hicho, lakini Allaah anakiondosha kwa utegemezi.”[2]

´Abdullaah amesema kuhusu hirizi na uchawi wa limbwata[3]:

“Ni katika shirki.”[4]

Ibn ´Abbaas amesema:

“Watu wanashirikisha kwa mbwa wao. Wanasema mbwa wetu anatulinda, lau si mbwa wetu basi tungeibiwa.”[5]

[1] Ahmad (23680).

[2] Abu Daawuud (3910), at-Tirmidhiy (1614), Ibn Maajah (3538) na Ahmad (3687) kupitia kwa Ibn Mas´uud na wengineo. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[3] Uchawi na vitu vingine ambavyo mwanamke hutumia ili mume wake ampende. Ibn-ul-Athiyr amesema:

“Imefanywa ni katika shirki kwa sababu ya kuamini kwao kwamba jambo hilo linaathiri na kufanya kazi tofauti na vile alivyokadiria Allaah.” 

[4] Abu Daawuud (3883), Ibn Maajah (3530), Ahmad (3615), at-Twabaraaniy (10503) na al-Bayhaqiy (19387) kupitia kwa Ibn Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Hakika matabano, hirizi na tiwalah ni shirki.”

Cheni ya wapokezi ya al-Haakim ni Swahiyh, kama nilivyobainisha katika ”as-Swahiyhah”.

[5] Ameipokea Ibn Abiy Haatim kupitia kwa Shabiyb bin Bishr: ´Ikrimah ametuhadithia, kutoka kwa Ibn ´Abbaas kuhusu maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

”… Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji, akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi msimfanyie Allaah washirika na hali ya kuwa nyinyi mnajua.” (2:22)

Cheni ya wapokezi ni dhaifu. adh-Dhahabiy amemtaja Shabiyb katika ”adh-Dhwu´afaa´” na akasema:

”Abu Haatim amesema kuwa Hadiyth zake ni laini. Ibn Jariyr amepokea kupitia kwake kutoka kwa ´Ikrimah pasi na Swahabah katika cheni ya wapokezi.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 72-74
  • Imechapishwa: 29/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy