3 – Madhambi yanayoitwa ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema katika usiku mmoja kuliponyesha:

“Je, mnajua nini Kasema Mola wenu?” Wakasema: “Allaah na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: “Katika asubuhi hii kuna baadhi ya waja Wangu wamepambaukia wakiwa ni wenye kuniamini na wengine wamekufuru. Ama yule aliyesema kwamba: “Tumenyeshewa mvua kwa fadhila na rehema ya Allaah”, basi huyo ndiye aliyeniamini Mimi na amekufuru sayari. Ama yule aliyesema ya kwamba tumenyeshewa mvua kutokana na sayari fulani na fulani, basi huyo amenikufuru Mimi na ameamini sayari.”[1]

“Msirudi baada yangu kuwa makafiri wapotevu baadhi wakizikata shingo za wengine.”[2]

”Mwenye kumwambia mwenzake ”Ee kafiri!”, basi ni lazima impate mmoja wao.”[3]

”Mwenye kumwendea kuhani au mpiga ramli ambapo akamsadikisha aliyoyasema, akamjamii mwenye hedhi au mwanamke kwenye tupu yake ya nyuma, basi amejiweka mbali, au ameyakufuru, yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[4]

´Abdullaah amesema:

”Kumtukana muislamu ni dhambi nzito na kumpiga vita ni ukafiri.”[5]

Baadhi wanasema kuwa maneno hayo yanatoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy (1038) na Muslim (71) kupitia kwa Zayd bin Khaalid al-Juhaniy.

[2] al-Bukhaariy (121) na Muslim (65) kupitia kwa Jariyr bin ´Abdillaah. al-Bukhaariy ameipokea tena kupitia kwa Ibn ´Umar, Ibn ´Abbaas na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhum).

[3] al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn ´Umar.

[4] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kupitia kwa Abu Hurayrah. Nimeipokea katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”, lakini pasi na ”mchawi”.

[5] al-Bukhaariy (48) na Muslim (64).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 70-72
  • Imechapishwa: 29/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy