Kiapo kilicho na kafara na kisicho nakafara

Kiapo chenye kuwajibisha kafara ni kiapo cha kitu kilicho mbele. Ama kiapo cha kitu kilichopita hakina kafara. Lakini hata hivyo ikiwa mwapaji amesema uongo anapata dhambi. Na ikiwa amesema kweli hana juu yake kitu. Lakini ikiwa mwapaji amesema uongo anapata dhambi. Na ikiwa amesema ukweli hana juu yake kitu. Mfano wa hili lau mtu atasema “naapa kwa Allaah sikufanya kadhaa”. Katika hali hii hana kafara ni mamoja ikiwa amesema ukweli au uongo. Lakini ikiwa ni kweli hakufanya, basi amesalimika na madhambi. Na ikiwa amesema uongo kwa maana ya kwamba alifanya, anapata dhambi.

Kiapo chenye kafara ni cha kitu kilichoko huko mbele. Mtu akiapa kwa kitu kilichoko mbele kwa kusema “naapa kwa Allaah sintofanya kadhaa”. Katika hali hii tunasema ukikifanya, basi juu yako una kafara. Usipokifanyahuna juu yako kafara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/532)
  • Imechapishwa: 29/06/2023