Kuhusu tafsiri ya kundi la pili na kwamba inahusiana na matishio na kuogopesha, ni miongoni mambo mabaya kabisa yaliyofasiriwa juu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Kusemwe vinginevyo nini kule kufanya maelezo kuhusu Allaah na kuhusu dini Yake kwamba ni matishio tu yasiyokuwa na uhakika wowote? Hili linapelekea kupinga adhabu zote. Kwa sababu ikiwa kunaweza kusemwa hivo juu ya adhabu moja tu, basi yanaweza vilevile kusemwa juu ya adhabu zengine zote.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 29/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy