Swalah ya aliyefanya Tayammum baada ya kutokwa na majimaji kwenye tupu yake

Swali: Wakati mwingine hutoka kwenye ncha ya uume maji meupe au maji kama gundi. Hufanya Tayammum kwa kutumia udongo. Kisha wakati wa swalah unafika akiwa bado yuko katika hali hiyo ya Tayammum. Kwa hivyo hufanya Tayammum na kuswali. Ninachokusudia ni kwamba yuko chooni. Je, swalah yake ni sahihi?

Jibu: Baada ya kamati kutafiti suala hili wamefikia kwamba: ni lazima kwa mwenye kutokwa na kitu katika uume wake ajisafishe kwa kutumia maji, kisha atawadhe. Ikiwa hatapata maji, basi ajisafishe kwa kutumia mawe yasiyopungua matatu mpaka asafishe sehemu hiyo, kisha afanye Tayammum kwa ajili ya swalah baada ya kuingia wakati wake.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/102-103)
  • Imechapishwa: 14/10/2026