Lazima kujisafisha kwa maji kila wakati wa swalah?

Swali: Je, mtu analazimika kujisafisha kwa maji kila mara anapotaka kutawadha?

Jibu: Si lazima kwake kufanya hivo kila anapotaka kutawadha. Bali analazimika kujisafisha kwa maji kwa kuosha sehemu yake ya mbele ikiwa ametokwa na mkojo au mfano wake, na huosha sehemu yake ya nyuma ikiwa ametokwa na kinyesi, kisha anatawadha kwa ajili ya swalah.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/102)
  • Imechapishwa: 14/10/2026